kwamamaza 7

Serikali ya Rwanda yatoa tangazo la kuuza mnada mali ya familia ya Diane Rwigara

0

Serikali ya Rwanda kupitia Bodi Kuu ya Kodi(RRA) imetoa tangazo la kuuza mnada baadhi ya vifa vya kiwanda cha Sigara  Premier Tobacco Company cha familia ya marehemu Rwigara Assinapol,baba yake Diane Rwigara.

Tangazo hili limetolewa baada ya mahakama ya kiuchumi tarehe 8 Machi 2018 kupiga marufuku rufaa ya hiki kiwanda kuomba mahakama kuachia huru badhi ya vifaa vyake maalum vilivyotaifishwa.

RRA ilisema kwamba mali  ya familia itauzwa mnada ili  kulipa kodi frw biliyoni 5 ambazo hiki kiwanda hakikulipa miaka iliyopita.

Haya ni baada ya mahakama ya Nyarugenge kupiga marufuku mashtaka ya hiki kiwanda kwamba utaifishaji wa vifaa vyake uliofanywa na RRA ulisababisha hasara kubwa.

Kiwanda hiki kilikuwa kikilipa frw miliyoni 200 za kodi kila mwezi na kutoa ajira kwa wafanyakazi 700

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.