kwamamaza 7

Serikali ya Rwanda yasikitishwa na kifo cha mfalme Kigeli

0

Serikali ya Rwanda inasema imepokea kwa masikitiko habari ya kifo cha leti Kigeli V Ndahindurwa, Mfalme wa mwisho wa Rwanda, aliyefariki dunia hapo juzi tarehe 16 Oktoba 2016 hospitalini Marekani, alikokuwa akiishi kama mkimbizi tangu mwaka 1992.

Serikali ya Rwanda kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema familia ya marehemu haijaijulisha serikali chochote kuhusiana na mipango ya mazishi, na kuongeza kuwa iko tayari kutoa uungaji mkono wake kuhakikisha mipango ya mazishi inanyooka endapo familia ya marehemu itawasilisha ombi hilo.

630x400-ct
Mfalme alifariki akiwa uhamishoni

Msaidizi wa karibu wa Mfalme Kigeli Boniface Benzige ameiambia BBC kwamba hadi sasa hawajaamua ni wapi na ni lini mwili wa mfalme huyo utazikwa.

“Hatujaafikiana kuhusu mipango ya mazishi yake. Kuna jamaa zake wanaoishi Afrika ambao lazima kwanza wawasili hapa, pia kuna washauri ambao tunashirikiana, hatujaamua la kufanya.”

Soma tena: Mfalme wa zamani wa Rwanda Kigeli V Ndahindurwa afariki

Amesema Mfalme Kigeli mara kadhaa alionesha nia ya kutaka kurejea nyumbani nchini Rwanda lakini hadi kufikia sasa haijafahamika ikiwa mwili wake utasafirishwa Rwanda.

Kabla ya kifo chake Mfalme Kigeli alitangaza kwamba bado yeye ni Mfalme wa Rwanda ijapokuwa nchi hiyo inafuata mfumo wa utawala wa jamuhuri.

Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 80, bila mke wala mtoto lakini wasaidizi wake wanasema wanafikiria kuhusu atakayerithi kiti cha Ufalme.

[ad id=”72″]

Kigeli V Ndahindurwa alipigwa marufuku nchini Rwanda na Mkoloni Mbeljiji mnamo Oktoba 1961, miaka miwili tu tangu aingie mamlakani baada ya Mfalme Mutara III Rudahigwa, kaka yake wa kambo, kufariki mjini Bujumbura alikokuwa amekwenda kikazi.

Haijajulikana kama atazikwa wapi ila Serikali ya Rwanda imesema iko tayari kutoa mchango wake kufanikisha shughuli hiyo.

Kigeli V Ndahindurwa kazaliwa mwaka 1936. Inasadikika amekufa kibudu kwani ni haramu kwa mfalme kuoa akiwa ugenini. Alitangazwa kuwa mfalme mwaka 1959 akiwa bado ni kapera mwenye umri wa miaka 23.

@Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.