kwamamaza 7

Serikali ya Rwanda inaazimishwa kuachilia ao kufikisha mahakamani Violette Uwamahoro

0

Jamii inayohusika na haki za binadamu (Human Rights Watch) imeomba serikali ya Rwanda kuachilia Uwamahoro Violette aliye kamatwa na polisi ao kumufikisha mahakamani.

Violette Uwamahoro, ni raia wa Rwanda anaye kuwa tena na uraia wa Uwingereza, wiki nenda ndipo polisi ilitangaza ya kuwa ilimukamata wakati yeye alikuja kusalimu familia yake.

HRW husema ya kuwa alikamatwa kinyume na sheria ya Rwanda hata kimataifa kwa sababu wakati mtu anakamatwa sherti ajulishwe ni nini anashutumiwa.

Kwa hayo pia jamii yake inajulishwa, msaidizi wake wa sheria na mahakama hupewa mashtaka anayo shutumiwa ili aweze azibiwa kufungwa ao kufunguliwa.

Msemaji wa polisi ya Rwanda Theos Badege alisema ya kuwa Uwamahoro alikamatwa baada ya kuwaarifu ya kuwa alihusika na makosa ya kujaribu kuwatafuta watu wa kuingiza katika chama cha RNC.

HRW husema ya kuwa bi Violette Uwamahoro alikamatwa kwa siri hadi wiki mbili, mtu aliye ongea naye wa nyuma ilikuwa tarehe 12 Februari 2017.

Mtu ambaye aliongea naye katika jamii, alikua akielekea katika kituo cha gari Kigali, baada ya saa chache simu yake kakosekana. Mume wa Uwamahoro, Faustin Rukundo ni mwana chama cha RNC, serikali huwashika kama chama cha ughaidi kwani wana chama huishi ukimbizini na wamoja walikuwa wana chama wa RPF.

Faustin Rukundo aliambia uandishi wa habari wa Uwingereza ya kuwa mke wake alitiwa mbaroni na ngazi za upelelezi Rwanda, na kuambatanisha na siasa na huo hukana kuwa mke wake ana husiana na mambo ya siasa.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.