Swahili
Home » Serikali ya Burundi yawataka raia kutofanya kazi nchini Rwanda”ile nchi haiwataki”
HABARI MPYA

Serikali ya Burundi yawataka raia kutofanya kazi nchini Rwanda”ile nchi haiwataki”

Waziri wa Sheria wa Burundi Aime Laurantine Kanyana jana amewataka wakazi kutotafuta kazi nchini Rwanda kutokana na kuwa Rwanda “haiwataki”. Haya ni baada ya takwimu kuonyesha kwamba Warundi 800 wamefukuzwa nchini Rwanda kwa mujibu wa Sauti ya Markani.

Huyu Waziri ametangaza haya katika hotuba yake ya kuanzisha madarakani Gavana wa mkoa wa Kirundo  Alain Gilbert Gatabazi, eneo la Gatare, wilayani Busoni.

“Jamani raia wa Kirundo, mtu anapokuangalia mno anakukumbusha kuvaa nguo(methali). Kwa nini mnatafuta kazi mahali ambapo hawawataki wakati ambapo kuna wanapowapenda na wanaweza kuwapatia kazi” Waziri Kanyana amesema

“Kule mnakokuenda na wakawafukuza bila kuwalipa, kwa nini hamfanyi kazi katika mikoa mingine wale ambao wana nguvu za kufanya kazi na akapata malipo yake bila wasiwasi” ameongeza

Waziri Kanyana amewaonya wakazi kwamba serikali haitaki kusikia  tena malalamishi ya Warundi kuhusu mali yao inayoachwa nchini Rwanda wanapofukuzwa.

“Hatutaki watu wanaovuka mipaka bila serikali kujua na kisha akaanza kulalamika kuwa ameiacha mali yake nchini Rwanda. Anaye shida ya kutafuta kazi anaweza kuwasiliana na uongozi kwa kutatua suala lake. Tunawataka kutii hili” Waziri Kanyana ameonya

Serikali ya Rwanda jumamosi imewarudisha kwao  Warundi 115 walioingia nchini kinyume na sheria.

Pia,jana terehe 29 Juni  Rwanda imewafukuza Warundi 200 kwa kusema wanaishi nchini kinyume na sheria.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com