kwamamaza 7

Serikali kuanza hesabu ya  wakimbizi asili ya DR Congo wanaotaka kurudi nyumbani katika kambi ya Kiziba

0

Serikali ya Rwanda imeweka wazi kuanza tukio la kuhesabu wakimbizi asili ya DR Congo wanaotaka kurudi nyumbani  leo tarehe 15 Meyi 2018 katika kambi ya Kiziba magharibi mwa Rwanda.

Kiongozi wa idhaa ya Wakimbizi kwenye Wizara ya majanga na Wakimbizi(MIDMAR),Jean Claude Rwahama amehakikisha tukio hili kwa kusema kwa sasa watu tisa kutoka kambi ya Kigeme,Mugombwa na Gihembe ndio waliosajiwa rasmi kuwa wanataka kurudi nchini DR Congo.

Huyu kiongozi amesema tukio hili litatekelezwa katika  kambi ya Kiziba ambako wakimbizi walionyesha hamu ya kurudi nyumbani.

“Baada ya kuhesabu wanaotaka kurudi nyumbani,kunatolewa,magari ya usafirishaji, ‘repatriation package’ kwa wakimbizi ili kuwasaidia kurudi kwao vyema.Hili linahitaji kujianda vilivyo lakini haitakuwa muda mrefu” Rwahama amesema.

Pia Serikali imewakumbusha watakaoamua kutorudi kwao kuendelea kutii sheria za nchi.

“ Wote walikuwa wakisema wanataka kurudi kwao,tutaona leo kama watakuenda wote ila  watakaobaki lazima kutii sheria kwani hatuwezi kuongoza watu ambao hawatii sheria za nchi” ameongeza

Wakimbizi katika kambi ya Kiziba walianza kupendekeza kurudi kwao tangu mwezi Februari baada ya vifo vya wenzao 11 juu ya maandamano.

Bonyeza hapa kupata habari zaidi

Ikumbukwe kwamba wakimbizi 44 walikamatwa na kufungwa jela kwa kudharau sheria za ndani ya nchi.

Kaimbi ya Kiziba inawahudhumia wakimbizi asili ya DR Congo 1700 tangu mwaka 1996.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.