Swahili
Home » Sekta ya Nishati ya maji katika miaka 7 ya muhula wa Rais Kagame
HABARI

Sekta ya Nishati ya maji katika miaka 7 ya muhula wa Rais Kagame

Kutoka mwaka wa 2010-2017 kipindi ambapo rais Kagame amekuwa akishika kiti cha urais wa Rwanda kwa muhula wa pili. Sekta ya nishati ilitiwa nguvu huku maji masafi akisambazwa kwa raia na mpaka sasa kiwango cha maji safi yanayopatikana ni m3 182 000 ikitoka 123 000 kwa siku mwaka wa 2010.

Asilimia 84.8 ya wanyarwanda hupata maji safi kulingana na sensa ya maisha bora ya nyumba ya mwaka 2013/2014 ikitoka asilimia 74.5 ya mwaka 2010 .

Na pia Shughuli za kuhifadhi maji zimeimarika sana kutoka kiwango cha asilimia 89 ya mwaka 2014 na asilimia 101 ya mwaka wa 2016. Hivohivo kiwango cha maji yanayopotezwa kilikwenda chini.

Mafanikio haya ya sekta ya Nguvu yalifikiwa kupitia ongezeko la Miundombinu husika na hasa kujenga viwanda vya kusafisha maji hapa kukijengwa viwanda pana kama Nzove II ambayo inatoa m 25 000 kwa siku kwa wakazi wa mji wa Kigali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kumejengwa viwanda vyingi nchini kote kwenye wilaya zote. Kwa mfano kampuni ya LVWASTAN II imejenga viwanda kwenye wilaya ya Nyanza ,Nyagatare na hata Kayonza ambacho kinatoa m3 10 210.

Vilevile wizara ya Miundombinu imesema kwa madhumuni ya kutolea suluhu tatizo la uhaba wa maji safi uliodumu kwa miaka kadhaa mjini Kigali, Serikali ya Rwanda ilisaini mkataba na kampuni ya “Cullingan International” na ambayo itashughulikia kiwanda cha Nzove II kukiongeza nguvu hadi kutoa m3 40000 za maji kwa siku. Na hata kukiongeza nguvu kiwanda cha Nzove I kutoka m3 40000 kwa siku hadi 65 000 kwa siku.

Hi itakuwa na lengo lakutolea suluhu la kudumu uhaba wa maji unaojitokeza mjini Kigali.

Serikali ya Rwanda imejipa lengo la kuongeza miundombini huku ile ya msingu kama maji na umeme vikiwekwa kipaumbele na sasa hata katika sekta ya umeme kuna imani ya kuwa mambo yatazidi kuwa mazuri kwa wanyarwanda kulingana na ongezeko lake.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter 

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com