kwamamaza 7

Sekta ya afya ilikuwa na badiliko kadhaa tangu RPF ishike madaraka

0

Maisha na ustawi wa Wanyarwanda ni baadhi ya wajibu wa serikali ya Rwanda inayotawaliwa na RPF kwa kipindi cha miaka 23 tangu kushinda vita vya ukombozi, RPF ilijitahidi kubadilisha maisha ya wanyarwanda hadi nchi za kigeni zijivunie mabadiliko hayo halisi.

Usidhani ni kuongeza chumvi kwa kuwa ikichukuwa mfano wa jinsi wagonjwa wa Ukimwi wanavyohudumiwa , na jinsi walivyogeuka kimawazo ,hali ya afya ya wanyarwnda unaona kwamba kuna mabaliko mazuri yaliyofanywa kwa kipindi cha miaka hiyo.

Serikali haikusimama kuomba msaada kutoka nchi tajiri na mashirika maarufu mfano wa Global Fund, huku ikiwa na madumuni ya kuwahudumia wagonjwa hadi nchi hizo na mashirika hayo waridhirike kwa jinsi wagonjwa hao wanaohudumiwa.

Mutu mmoja aliefanya kazi katika idara ya kupambana na virusi vya ukimwi, muda si mrefu baada ya Mauaji ya Kimbari, aliambia Bwiza.com,huku machozi yakimtoka akisimulia jinsi serikali ilivyofanya jitihada ikitaka kuwapatia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Alisema “Serikali ilipigana katika vita hivi baada ya vile vya risasi. Nyakati hizo watu walikuwa wakifariki kila siku, wakati ambapo hawajakuwa wakaelewa lengo la hizo dawa , ielewekwe na hizo hazikuwa nyingi lakini hadi sasa watu walikwisha elewa umuhimu wake na kuzichukuwa bila wasiwasi,huwo ni kama ushindi, nakumbuka awali serikali ilikuwa ikiwapatia hata chakula lakini mawazo yalikuwa yale yale.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mabadiliko kwa ujumla

Mabadiliko hayo yanayohesabiwa kutoka miaka 20 yanahusu maendeleo ya sekta ya afya Kiganga ambako kuna nyakati ambazo mtu angehitaji kutibiwa kwa upasuaji kwa leo haiku mhimu .

Wakati ambako Waziri Mkuu, Anastase Murekezi, alipokuwa akihotubia mbele ya bunge alisema kuhusu mabadiliko yaliyofanywa kwenye sekta ya afya, akisema kwamba utoaji huduma ulisaidia sana kuendeleza maisha bora ya wanyarwanda.

Takwimu kutoka Benki Kuu ya Dunia, zaonyesha kwamba kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita, matumaini ya kuishi kwa wanyarwanda yaliongezeka mara tatu ikiwa miaka 28 mwaka 1994, ikabadilika 46 mwaka 2000, na 66 katika mwishoni mwa mwaka 2015.

Idadi ya miundombinu ya sekta ya afya nayo iliongezeka kwa kuwa kulijengwa vituo vidogo vya afya 406, vituo vya afya 499, na Hospitali za Wilaya 36 na hata hospitali kuu 7.

Kulichaguwa wahudumu wa afya kwa kila kijiji/vileji ambao wanatoa ushauri wa kiafya kwa wananchi, wakawaletea huduma za haraka za matibabu, jinsi ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza, kupamba na kilisho duni hususani cha mtoto na mamake.

Wahudumu hao walifanya kupunguka kwa idadi ya wazazi wanaofariki wakati wa kujifungua kutoka 1071/100000 mwaka wa 2000 , wakawa 476 mwaka wa 2010, hadi 210 mwaka wa 2015. Kulikuwa pia na ongezeko la idadi ya watoto wanaozaliwa hospitalini hadi 90%.

Rwanda ilianza pia teknolojia ya kutumia ndege zisizokuwa na madereva kwa kusafirisha damu.

Kuhusu malengo ya millennia Rwanda iliwahi kutekeleza lengo la nne na la tano za Kiafya zinazolenga kupungua idadi ya watoto na wazazi wanaofariki wakati wa kujifungua.

Ulipaji wa bima za kijaami (mituelle de santé) inayosaidia wananchi kupata huduma za kiafya uliongezeka kutoka 44% mwaka wa 2005 hadi 81,6% mwaka wa 2015.

Kuhusu kupampana na magonjwa kama malaria , wananchi walipewa viandarua kwa kiwango cha 80%

Wahudumu wa afya wanahesabiwa kuwa 45,516. Kuhudumia kwa moja kwa moja wanawake wajazito kunahesabiwa kuwa 99%, wakati utoaji wa chanjo ukihesabiwa kwa 93%.

Watoto na watu wazima 80% wanapata dawa za kupungua makali ya virusi vya ukimwi

Huduma hizi zinaendeshwa moja kwa moja sera wa kutahiri wanaume unaosaidiwa pia na kazi zinazofanywa na wanajeshi ijulikanayo kama (army week)

Serikali ilianza pia kuwalipia gharama za matibabu watu wasiojiweza ambao wana magonjwa ya hatari wanaotaka kupata matibabu kutoka nchi za ng’ambo

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.