Home HABARI MPYA Sababu zilizowafanya viongozi watano wa REB kufukuzwa zatiwa hadharani
HABARI MPYA - April 12, 2018

Sababu zilizowafanya viongozi watano wa REB kufukuzwa zatiwa hadharani

Waziri wa elimu Dk.Eugene Mutimura asubuhi hii ameweka wazi sababu iliyowafanya viongozi watano wa Bodi Kuu ya Elimu(REB)  kufutwa kazi kama ilivyotangazwa  jana na uamuzi wa mkutano wa mawaziri.

Waziri Mutimura  ameeleza kuwa viongozi hawa  wamefukuzwa kutokana na kutotimiza wajibu wao vilivyo kwa maendeleo ya elimu.

Dk.Mutimura ameeleza kwamba hawa walishindwa kutatua suala la kuchelewa kutoa shahada na stashada kwa wanafunzi wanaomaliza masomo yao na kuwa zinaandaliwa  ugenini kinyume na lengo la Bodi Kuu ya Elimu(REB).

Pia Waziri ameeleza sababu nyingine ni kuchelewa kutoa vitabu vya wanafunzi ambako vilikuwa vikimaliza kama miezi nane njiani.

Waliofukuzwa ni Dk. Joyce Musabe ambaye alikuwa Mkurugenzi wa tawi la mambo ya masomo, Dk. Tusiime Rwibasira Michael ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa tawi la mitihani na mazoezi waliofukuzwa , Mujiji Peter ambaye alikuwa Afisa mkuu kwa wajibu wa kazi za ujumla, Karegesa Francis  ambaye alikuwa mkurugenzi wa tawi la mali na Bagaya Rutaha ambaye alikuwa mkurugenzi wa tawi la kutoa biashara.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.