kwamamaza 7

Sababu za Wanyarwanda kukamatwa nchini Uganda zajulikana

0

Baada ya visa kadhalika  vya kuwakamata  Wanyarwanda nchini Uganda kuenea,sababu zinazosababisha vitendo hivi zimejulikana.

Taarifa za Virunga Post zimefafanua kuwa Wanyarwanda waliokamtwa na maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI ni wale ambao ni vipingamizi na wapinzani wa mipango ya chama cha Rwanda National Congress,RNC nchini Uganda.

Mmoja mwa wakristo wa kanisa la AGAPE,mjini Mbarara ambapo ni mahali panapotuhumiwa kuwa kiota cha kusajili wanajeshi wa RNC,ametangazia hiki chombo cha habari kuwa hawa Wanyarwanda hushtakiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda kisha wakakamatwa na kuteswa kimwili na maafisa wa upelelezi wa Uganda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwingine ambaye hakutaka jina lake kutambulika ameeleza kwamba huu ni mkakati wa RNC ili kuweza kuendelea na mipango yao ya kusajili wanajeshi bila kipingamizi chochote.

Pamoja na haya,Wanyarwanda karibu elfu walikamatwa na kufungwa nchini Uganda kwa kushtakiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda na ni baada ya hivi karibuni Mnyarwanda Emmanuel Cyemayire kutekwa nyara mjni Mbarara na kupelekwa mahali pasipojulikana kwa sasa.

Kwa upande wa serikali ya Uganda walisema kuwa Wanyarwanda wanaokamatwa ni wale wenye uhusiano na vitendo vya ugaidi nchini Uganda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.