Swahili
HABARI MPYA

Rwanda:Waziri wa miundo mbinu ashtakiwa kufanya  ngono

Waziri wa miundo mbinu James Musoni ameshtakiwa na mwanamume kwa jina la Rtd.Capt. Patrick Safari,47, kumpokonya mwanamke wake kwa jina Imaculee Kayitesi aliyemuoa mwaka 2010.

Rtd.Capt.Safari Patrick ameelezea Igihe.com kwamba alimuoa Kayitesi mwaka 2010 baada ya kifo cha mke wake aliyeacha watoto watatu kisha akaenda shuleni nchini Uganda na kuwa wawili walijifungua mtoto mmoja.

Alipokuwa Nchini Uganda Safari ameeleza kwamba alisikia fununu nyingi kwa majirani zake kuwa kuna mume mwingine ambaye anakuja nyumbani kwake kisha akamua kutafuta namna ya kupata habari za kutosha kuhusu hili kwa kuwa mke wake alikuwa akikanusha kila mala alipoulizwa kuhusu hili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Nilijua kwamba kuna mwanamume anayekuja kwangu wakati wa  usiku na wikendi ila mke wangu aliniambia kuwa ni marafiki wa familia yangu”Safari amesema

Aliwahi kuniomba nambari ya simu ya waziri Musoni nikampa kwani nilifikiri kwamba ni sababu za kikazi.Nilijua baadaye kwamba walikuenda kutembea kule mbuga ya Akagera”ameongeza

Huyu mwanamume kupitia sauti yenye  huzuni amesema kwamba ana uhakika wa jambo hili kwani aliwataka wafanyakazi  wake kumpa habari zote husika kisha mmoja wao alimunyoshea kidole alipomuona waziri Musoni kwenye TV.

Bw Safari amehakikisha kwamba  Waziri Musoni alimpachika mimba mke wake na kusababisha hasara kubwa kwa kuwa familia hii ilishindwa kulipa deni la benki sawa na  frw miliyoni 40 pamoja na kukataliwa kuja nyumbani kwake hadi alipoenda kulala hotelini.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pengine ameeleza kwamba kutokana na  hili nyumba yake yenye bei frw miliyoni 106 iliuzwa mnada frw miliyoni 51 na kuwa anaishi katika hali mbaya ya kulea watoto watatu.

Waziri  James Musoni hajafunguka lolote kuhusu haya madai.

Waziri James Musoni angali katika serikali ya  Rwanda tangu mwaka 2005 ambako aliongoza wizara mbalimbali.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com