kwamamaza 7

Rwanda:Wapinzani watoa ahadi ya kurudisha mali ya familia ya Rwigara na ya tajiri Rujugiro.

0

Kwenye maandalizi ya kushambulia Rwanda,wapinzani wameahidi kurudisha mali yote  ya familia ya Assinapol Rwigara na ya tajiri Ayabatwa Tribert Rujugiro baada ya kupata ushindi wa kuipindua serikali ya Rwanda.

 Kupitia barua yake ndefu,aliyekuwa mwendeshamashtaka mkuu kwenye serikali ya Rwanda iliyo ukimbizini, Abdallah Akishuli ameeleza  kwamba familia ya Assinapol Rwigara itarudishiwa  nyumba  yao iliyobomolewa pamoja na fidia sawa na bei yake.

Pia barua hii inaeleza kwamba tajiri Rujugiro Tribert Ayabatwa  atarudishiwa jumba lake la kifahari kwa jina ‘Union Trade Center’ maarufu kama UTC lililoko mjini Kigali.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Barua hii imeongeza kuwa wenyeji wa hoteli Top Towers watalipwa fidia sawa na bei ya jumba lao lililobomolewa.

Pamoja na haya, Wapinzani wa serikali ya Rwanda wameanza maandalizi ya kukusanya fedha zitakazosaidia katika vita vya kuishambulia nchi kupitia dhamana(bonds) zenye bei Euro miliyoni 10.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.