Swahili
HABARI MPYA

Rwanda:Wakimbizi watano asili ya Congo wauawa  katika maandamano

Raia wa Congo aliyeuawa/picha na Victoire Murwanshyaka/hisani

Wakimbizi watano asili ya DR Congo wameuawa katika maandamano Kwenye ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuhudhumia waakimbizi,UNHCR nchini Rwanda wilayani Karongi.

Msemaji wa polisi ya Rwanda,CP Theos Badege ameambia vyombo vya habari kwamba wanausalama wametumia nguvu ili kujadili na hawa wakimbizi.

“ Wakimbizi wametupia polisi mawe na walikuwa na vyuma” CP Badege ameeleza

Pia huyu afisa wa polisi amesema kwamba wakimbizi 20 na polisi  saba wamejeruhiwa, wakimbizi 15 wamekamatwa na watano wamefariki.

Polisi imefafanua kuwa tukio hili ni baada ya hawa wakimbizi kukataa kurudi katika kambi yao ya Kiziba na kuwateka nyara baadhi ya wafamyakazi wa UNHCR.

Pengine kuna taarifa kwamba 22 wamefariki kwa kupigwa risasi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakimbizi walianza maandamano jumanne wakipiga marufuku upunguzaji wa chakula kutoka frw 7500 hadi 5700 kila mwezi pamoja na kutoa ombi la kuhamia nchi nyingine ama kurudi kwao.

Wakimbizi maelfu 16 wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Kiziba tangu miaka 20 iliyopita.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com