kwamamaza 7

Rwanda:Wakazi watangaza wasiwasi kufuatia kodi za ardhi

0

Wakazi wameweka wazi kuwa na wasiwasi kutokana na kuwa suala la kulipa kodi za ardhi kwa kueleza kwamba hawana uwezo.

Wakizungumza na VOA, baadhi ya wakazi hawa wamesema kuwa kutoa kodi ni jambo muhimu ila kikwazo ni kwamba baadhi yao hawana uwezo wa kulipa kodi hizi.

Mmoja wao ameleza kuwa jambo la kulipa kodi ni kikwazo kikubwa kwa watu wasio na uwezo.

Huyu amesema”Unapochunguza unaona kwamba kodi za ardhi hazihusiani na ukubwa wa ardhi na hana mapato mengine,hili linasababisha wakazi kushindwa kulipa kodi”.

Mwingine amependekeza kuwa serikali ingelichunguza tena hili  ili kurahisisha kodi kwa watu wasio na uwezo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kamishna makamu kwa wajibu wa kodi za ngazi za chini,Erneste Karasira amewaomba wakazi wasio na uwezo wa kulipa kodi za ardhi hawana budi kuwasilisha suala lao kwenye baraza la mashauri wa wilaya waishimo kulingana na kanuni husika.

Wakazi wanaeleza kutokua wa na uwezo wa kulipa kodi za ardhi ila Ofisi kuu ya kodi nchini(RRA) inatarajia kupata frw bilioni kumi kwenye mwisho wa mwaka huu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.