kwamamaza 7

Rwanda:Wafanyakazi wenye vyeo vikubwa asili ya Uganda,wafukuzwa kazini

0

Taarifa za Chimpreports zinasema kuwa wafanyakazi wenye vyeo vikubwa asili ya Uganda wamefukuzwa kazini kwa sababu zisizoeleweka kwao.

Baadhi ya hawa kuna Vivian Igunduura aliyekuwa meneja mkuu makamu wa benki ya Ecobanque ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini.Huyu aliambiwa kuwa uamuzi wa benki ni kuwa mkataba wa kazi yake utamalizika mwezi Octoba bila kumueleza sababu ya jambo hili.

Mwingine ni Beatrice Kibwika Kantono aliyekuwa na nafasi ya teknolojia na kujikinga majanga aliyetakiwa kujiuzulu katikati mwa mwezi Septemba na kuelezewa kuwa kazi yake haihitajiki kamwe.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia Ojonjoro aliyekuwa mfanyakazi wa benki kuu ya nchi(BNR) mkataba wake ulimalizika mwezi Septemba na kuwa raia wa Uganda wawili walikuwa wafanyakazi wakuu wa Rwandair kuambiwa kuwa mkataba wao wa kazi hauataboreshwa tena.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mkuu wa mambo ya kidiplomasia kwenye waziri ya mambo ya nje mjini Kampala,Margaret Kafeero ameleza kuwa anatarajia kujua mapana na marefu kuhusu jambo hili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya Chimpreports kutangaza kuwa kuna vita baridi kati ya Rwanda na Uganda juu ya usalama na ulinzi,upelelezi na miradi ya miundo mbinu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.