kwamamaza 7

Rwanda:Vijana watangaza uhaba wa kondomu hasa vijijini

0

Kijana mmoja kutoka wilaya ya Gakenke na mwenzake kutoka wilaya ya Rubavu wa wakizungumza na VOA,wamesema kuwa kunahitajika namna ya kusafirisha kondomu hadi vijijini na kuongeza kuwa haina budi kutoa kondomu kwa bure kwa kuwa ni kikwazo kwa vijana kuinunua dukani kwa kuwa kuinunua  faranga hamsini, bei ambayo wanasema kuwa ni ghali kwao.

Suala hili ni kinyume kwa vijana wanaoishi mjini kwa kuwa kuna vijumba vya kutoa kondomu kwa bure kwa wanaohitaji huduma hii hata kama vijana wanalalamika kuwa hawapati idadi wanayohitaji.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Afisa mmoja kwa wajibu wa kutoa kondomu kwenye vijumba hivi, amepiga marufuku madai ya vijana hawa kwa kueleza kuwa kuna baadhi ya vijana ambao hutaka kupata zaidi ya idadi ya kondomu nne walizokubaliwa na serikali.

Ofisi kuu ya afya,RBC imetangaza kuwa hununua idadi ya kondomu inayotosha kila mwaka ila tatizo ni namna ya kusafirisha kondomu hizi nchi popote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Afisa wake,Anicet Nzabonimpa ameleza kuwa kuna mahali kunakokosekana kondomu kwa kuwa ni vigumu kusafirisha kondomu unapolinganisha na dawa na kuwa kunatarajiwa namna ya  kutatua suala hili kama vile kuungana mkono na mashilika binafsi,wilaya,tarafa na vijiji ili kusafirisha kondomu.

Nchini Rwanda,kunatumiwa kondomu 10,000 hasa zile za wanaume kila mwaka.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.