kwamamaza 7

Rwanda:Serikali yaruhusu wakazi kumiliki bunduki

0

Wizara ya haki imetangaza imefkisha bungeni sheria itakayo waruhusu Wanyarwanda kumiliki siraha kama vile bunduki.

Waziri Johnston Busingye ameelezea Watangazaji kuwa  hata kama sheria hii imeanzishwa haimanishi kuwa bunduki zitazagaa nchini kote kwani ni nadra kutimiza sheria na masharti yote ya kumiliki bunduki.

Kuria: Waziri wa Haki Johnston Busingye na makamu wake Evode Uwizeyimana akielezea watangazaji

“Haitakuwa rahisi kwa yeyote kumiliki bunduki kwani kuna orodha ya mashariti ni ndefu mno.Ni kama kusema haiwezekani.Ni kama ngamia kupitia kishimo cha sindano.Uwepo wa sheria hii ni kwa matumizi itakapohitajika”

Waziri Busingye amesisitiza haistahili kuleta hofu hadaharani kwani serikali haiwezi kuamua jambo ambalo linaweza kutia hatarini wakazi wake.

Sheria husika na silaha ilianzishwa nchini Rwanda mwaka 1979 na kuboreshwa mwaka 2009.

Fred Masenegsho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.