kwamamaza 7

Rwanda:Serikali kuuza mnada mali ya familia ya Rwigara mwezi huu

0

Ofisi kuu ya kodi nchini,RRA imehakikisha kuuza mnada mali ya familia ya Assinapol Rwigara mwezi huu wa Februari 2018 kutokana na kuwa familia hii hakulipa kodi  Frw  biliyoni 5 na miliyoni 600.

Ofisi hii imeeleza kwamba imeanza kuhesabu gharama ya mali iliyotaifishwa ili kupata malipo hata kaa mnada ulichelewa.

Mkurugenzi wa RRA,Richard Tushabe ametangazia VOA kuwa huu mnada ulichelewa juu ya ufuatiliaji wa kanuni husika.

Richard Tusabe amesema”Mnada ulichelewa kutokana na kuwa inabidi kufuata kanuni husika,wenyeji wa kampuni ya cha Premier Tobacco walikuwa na madeni mengi hasa benki.Tuko tayari kuunga mkono wale wote husika na hili mwezi huu wa Februari kurudisha fedha hizi kwa kuwa ‘procedures’ zitakuwa zimemalizika”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wanafamilia hawakutaka kuongea kuhusu mali yao iliyotaifishwa ila  wachambuzi wa suala la familia hili wametangaza hata kama hawajui mali yote ya familia hii ila baadhi ya mali yao iliyoko nchini ilikabiliana na vikwazo kama vile nyumba zilizobomolewa,utaifishaji wa akaunti za benki na kukoma kuendelea kwa kazi za Kiwanda cha sigala,Premier Tobacco na mengine.

Kwa hiyo,wachambuzi wameeleza kwamba haya yaliathiri mno mali ya familia hii.

Assinapol Rwigara alifariki mwaka 2015, bi Rwigara Adeline Mukangemanyi Rwigara na binti yao Diane Rwigara wangali gerezani kwa kushtakiwa uchonganishi, uchochezi wa kikabila namatumizi ya hati bandia.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.