Swahili
HABARI MPYA

Rwanda:Safari za kutibiwa mafigo ugenini karibu kufupishwa

Mgonjwa akitibiwa ugonjwa wa mafigo

Safari za kuenda kutibiwa mafigo katika nchi za nje zinakaribia kufupishwa kwa Wanyarwanda,ni baada ya wanafunzi 7  kumaliza masomo ya uganga unaohusiana na mafigo kuenda kujiozeza tena nchini Uhindi  ambayo ni mahiri kwa ufundi huu.

Akitangaza habari hizi,waziri wa afya Dkt Diane Gashumba amesema kuwa wanafunzi hawa watasaidia sana watu wenye ugonjwa wa mafigo na kuwa kuna mpango wa kuanzisha hospitali bora ya kutibu mafigo na kupandikiza yaliyoharibika kwa msaada wa wekezaji kutoka Uhindi na Marekani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri Gashumba ameongeza kuwa nchi hii inahitaji mchango wao wa kutibu mafigo na kujikinga ugonjwa huu na kuwa hii ni bahati kubwa.Kwa upande wa wanafunzi wamesema kwamba safari yao italeta manufaa ya kuboresha uganga wa mafigo,akizungumza na RBA,mmoja amesema kuwa anajianda kutia mkazo mambo ya kupandikiza mafigo.Mwenzake amesisitiza kuwa jambo muhimu ni kutoa huduma nzuri,kusaidia kimaoni wagonjwa na wasiwo kwa kuwa kuna fununu za kuwa kumpa mtu figo hubaki maisha maovu.

Wanafunzi wakiwa na viongozi tofauti akiwemo Waziri wa afya,Dkt.Diane Gashumba

Pia,Waziri Gashumba amekumbusha Wanyarwanda kujilinda kwa kutokula mafuta mengi,sukali na kufanya mazoezi kwa kuwa ugonjwa huu unatibiwa kwa bei ghali na ni bora kujikinga kuliko kutibiwa kwa kusema”Magonjwa haya yasiyoambukizwa yanazidi kuenea dunia nzima,tunahamasisha watu kujilinda vilivyo”.

Nchini Rwanda kuna hospitali 5 za kutibu wagonjwa wa mafigo zenye mashine za kuyasafisha  yakiwemo CHUB,CHUK,Gisenyi,Gihundwe na kuna mpango wa kuanzisha nyingine Kanombe.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye 

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com