Swahili
Home » Rwanda:Mamba wazidi kuua walowezi karibu na Nyabarongo
HABARI MPYA SIASA

Rwanda:Mamba wazidi kuua walowezi karibu na Nyabarongo

Idadi ya walowezi wa karibu na mto wa Nyabarongo wanaouawa na mamba inaongezeka kila siku,ni baada ya kuwaua watu 8 katika wilaya ya Kamonyi na Nyarugenge mwezi huu.

Walowezi wakitupa jicho kwenye tukio la kumuua mwenzao

Walowezi wa sehemu hii wanasema kwamba mamba hawa walitiwa na serikali mtoni wa Nyabarongo ili  washambulie samaki wakubwa ambao walikuwa wakikula wadogo na kupunguza mavuno ya samaki lakini mamba hawa hawakuishi mtoni baali walijifisha katika nyasi za pwani na kuanza kula watu wanaokaribia hapo. Karibu hivi jana mamba alimuua mwanamke aliyekuwa akitafuta nyasi na  Habamenshi Oreste siku mbili kabla,Tugirimana Jean Pierre  tarehe 12 Agosti na Nyirampakaniye Sperata mwezi wa July 2017.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande wa uongozi wa wilaya ya Nyarugenge,Kayisime Nzaramba amesema kuwa wanyama na maisha ya binadamu ni lazima kulindwa vilivyo kwa kusema”Pia maisha ya binadamu naya wanyama hawa wanaokaribia kufifia walindwe sawa”.

Walowezi wakijaribu kumunusuru mwenzao kwa kutuia mashua

Haya ni madai ambayo walowezi wanajibu kwa kusema kwamba itaibidi serikali kulipa fidia za watu wanaokufa,mmoja amesema”Akimuua mtu,basi serikali ilipe fidia familia ya malehemu”.

Mwanamke akihuzunishwa na kushindwa kumsaidia mwenzake

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com