Swahili
HABARI MPYA SIASA

Rwanda:Madai kinyume kati ya chama cha upinzani FDU na ofisi kuu ya magereza kuhusu hali ya maisha ya Victoire Ingabire

Spika wa chama cha upinzani FDU-Inkingi ulaya,Justin Bahunga ameweka wazi kwamba  mwenyekiti wa chama Victoire Ingabire Umuhoza ametimiza wiki nzima bila kupata chakula.

Kupitia tangazo lake, Justin Bahunga ameleza kwamba Victore Ingabire amekosa chakula baada ya baadhi ya washiriki wa chama chake waliokuwa walimletea chakula kukamatwa na polisi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Justin Bahunga amendelea kwa kusema kwamba kuna wasiwasi za kutojua hali ya maisha ya Ingabire na kuwa wanafikiri kwamba anaweza kufa kwa njaa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande mwingine,Spika wa ofisi kuu ya magereza(RCS),CIP Hillary Sengabo ameambia BBC kuwa Ingabire yu hali nzuri na kuwa anakula chakula kama kile cha wafungwa wenzake wenye msokoto na kuwa Ingabire ameishatoa jina la mtu mwingine atakayendelea kumletea chakula kama kawaida.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ingabire Victoire Umuhoza alihukumiwa miaka 15 gerezani mwaka 2010 baada ya kushtakiwa uchochezi,kukana mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com