Swahili
Home » Rwanda:Chama cha upinzani FDU-Inkingi chatoa maoni kuhusu viongozi wake waliokamatwa
HABARI MPYA SIASA

Rwanda:Chama cha upinzani FDU-Inkingi chatoa maoni kuhusu viongozi wake waliokamatwa

Spika wa chama cha FDU-Inkingi,Bw Justin Bahunga

Spika wa chama cha FDU-Inkingi,Justin Bahunga kupitia tangazo akiwa ukimbizini kule Uingereza ameleza kwamba kuwakamata viongozi  wa chama ni kitendo cha kuwatia uoga wafuasi.

Spika wa chama cha FDU-Inkingi,Bw Justin Bahunga

Ameongeza kwamba kitendo hiki kutokea baada ya kuikamata familia ya Diane Rwigara kinadhamiria kuwanyamazisha wapinzani wa serikali nchini Rwanda.

Pia,chama kingine cha upinzani kisichokubaliwa kufanyia siasa nchini  Rwanda kwa jina PDP-Imanzi kimetangaza kuwa kiongozi  makamu wake,Jean Marie Vianney Kayumba amekamatwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na hayo,polisi iliwakamata watu saba akiwemo kiongozi makamu wa FDU-Inkingi,Bw Boniface Twagirimana na wenzake  wanne wa chama cha FDU-Inkingi wakituhumiwa kujiunga na wanamgambo katika nchi jirani isiyotajwa majina.

Kiongozi makamu wa Chama cha upinzani,FDU-Inkingi,Bw Boniface Twagiriamana

Haya yamethibitishwa na spika wa polisi,ACP Theos Badege

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ni baada  ya kumshitaki kiongozi wa FDU-Inkingi,Victoire Ingabire kuwa na ushirikiano na FDLR .

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com