kwamamaza 7

Rwanda:Chama cha upinzani chailaumu serikali baada ya viongozi kuamrisha wakazi kukata mazao yao kwenye ha 30

0

Chama cha upinzani Democratic Green Party of Rwanda (DGPR) kimelaumu viongozi wa ngazi za chini wilayani Kirehe tarafani Nasho mashariki mwa nchi baada ya amri iliyotolewa kwa wakazi kuharibu mihogo,maharagwe na mtama karibu ha 30 ambako viongozi wanasema hakuluhusiwi kupandwa mazao kwa kuwa ardhi ilie ilikuwa ya mifugo.

Mwenyekiti na Mkurugenzi wa DGPR, Dk.Frank Habineza ametangazia Sauti ya Marekani kuwa viongozi wa ngazi za chini ndio ambao wenye hatia kwani hawakufanya ufuatiliaji wa mambo yanayoendelea wanapoongoza.

“Hili ni jambo la kusikitisha sana, baya,halistahili kutokea.Wakazi walilima viongozi wakiangalia na sasa wanawaambia kuharibu mazao yao.Inastahili viongozi walipe fidia ya mazao ya wakazi”

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Mtama huo ulikuwa karibu kuvunwa,wanageliwakataza kabla,inaonekana waziwazi kuwa viongozi walishindwa kutimiza wajibu wao,viongozi wana wajibu wa kuwakinga wakazi kufanya makosa.Haya ni sawa na vile vya kubomoa nyumba za wakazi mjini Kigali”ameongeza

Dk.Frank Habineza ameeleza serikali inastahili kuwaachia hii ardhi kwani hakuna ng’ombe huko na kisa hiki ni tokeo la kuwa wakazi hawana mashamba ya kulima.

Hili ni suala pia mbali na kuwa eneo hili kuna njaa,serikali haina budi kuwapatia wakazi ile ardhi kwani miaka kama nane imemalizika bila ng’ombe huko”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katibu mtendaji wa tarafa ya Nasho,Console Kanzayire alitangazia Radiyo Izuba wakazi waliamrishwa kutolima ardhi ile kupitia mkutano ila walipofika nyumbani walifanya kinyume.

“Tulikuwa tukifikiri kwamba hawa wakazi wamesikiliza kwa makini waliyoambia tuliopuwa katika mkutano lakini walifanya kinyume na amri ya hati ya wilaya ya kuwa hawaluhusiwi kulima ardhi ile”

Eneo la mashariki mwa Rwanda ni moja mwa maeneo ambayo hukabiliwa na jua kali na mala nyingi serikali huwatunza wakazi kwa kuwapatia vyakula.Wakazi walitangaza kwamba tukio hili ni dahalili ya kuwa watakumbwa na njaa siku za usoni.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

[xyz-ihs snippet=”google”]

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.