kwamamaza 7

Rwanda:Asasi za kiraia zailaumu serikali kuhusu suala la kuhamisha wakazi

0

Utafiti wa taasisi ya utafiti,IRDP umeonyesha kwamba serikali haikutoa muda wa kutosha kwa wakazi ili wajiande vilivyo namna ambavyo watahama pia na kuwalipa fidia kulingana na kanuni.

Utafiti huu ulionyesha kwamba wakazi walisema kuwa hawakujadiliana na serikali bali waliamrishwa kukubali fidia bila kusita.

Mmoja wao,Theogene Higiro ambaye ni mkazi wa wilaya ya kicukiro,mashariki mwa mjini Kigali, eneo la Gahanga kunakotarajiwa kujengwa uwanja wa mpira, amesema kuwa walishangazwa na kuona kuwa kwao kutajengwa uwanja wa mpira bila kujua .

Kiongozi wa IRDP,Eric Ndushabandi ametangazia The East African kuwa wakazi wengi walihamishwa bila kujua mengi husika na jambo hili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ripoti hii ya utafiti huu inaonyesha kuwa 27% za wakazi walisema kuwa walijua kwamba watahama ila 3% walisema kuwa walikuwa hawajui lolote kuhusu jambo hili.

Mala nyingi wakazi husikika wakilalamikia mambo husika na uhamiaji kutokana na kuwa viongozi hawafuatilii kanuni za jambo hili hasa kulipa fidia na bei yake.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.