Swahili
HABARI MPYA SIASA

Rwanda yatarajia mapato ya miliyoni $64 kutoka mikutano ya kimataifa mwaka huu

Ofisi ya maendeleo ya utalii kupitia mikutano nchini Rwanda imetangaza kuwa mwaka jana ilipata miliyoni $47 kutoka mikutano 42 na kuwa wanatarajia kupata millyoni $64 kutoka mikutano 55 itakayoipokea mwaka huu wa 2017.

Rais wa Tchad,Idriss Derby akiwahutubia washiriki wa AU mwaka 2016 mjini kigali

Ofisi hii imeweka wazi kuwa fedha za kigeni kutoka mikutano ya kimataifa wa kati wa miaka 5 ziliongezeka kiwango cha 25% kwa sababu ya maandalizi na utoaji wa huduma nzuri kulingana na taarifa ya RBA.Kiongozi wa mpito wa RCB,Frank Murangwa amehamasisha raia wa Rwanda kuwakaribisha vizuri watalii wanaokuja nchini Rwanda ili waweze kupata manufaa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Serikali ya Rwanda ilianzisha mkakati wa miaka 7 wa kupanua utalii kwa kutia nguvu sana mambo ya kuhudhuru mikutano ya kimataifa,mahojiano na mambo mbali mbali MICE(Meetings,Incentives,Conferencies and Events) mwaka 2014.

Hoteli Radisson Blu inayokaribisha wageni wengi

Mkakati huu ndio uliowezesha Rwanda kupata miliyoni  $ 39 mwaka 2015 kutoka $ 29 mnamo mwaka 2014 na kuna lengo la kupata miliyoni $207 mwaka 2018 kwa kuwa miundo mbinu ilitiliwa mkazo kama vile hoteli Marriot,Nobilis,Sheraton,Zinc Kigali Hotel,Radisson Blu Hotel na nyingine.

Hoteli Marriot mjini kigali

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com