kwamamaza 7

Rwanda yataka Warundi wanaotuhumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbali kufika mahakamani

0

Ofisi kuu ya Mwendeshamashtaka nchini Rwanda imeeleza inataka Warundi wanaotuhumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda mwaka 1994 kufikishwa mahakamani.

Mwendeshamashtaka Mkuu  kwa wajibu wa ufuatiliaji wa uhalifu wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda, Jean Bosco Siboyintore jumatatu wiki hii, alieleza mpango huu unakabaliana na tatizo la kuwa siyo rahisi kuwa na uthibitisho kamili wa kuwa hawa raia waBurundi walishiriki  katika mauaji ya mbali nchini Rwanda.

“ Mahali kama Ntongwe, Rilima na Nyakizu na kuwa  ni vigumu kuwakuta hawa wanaozungumziwa katika hizi kesi. Kwa mfano, Macumi, Murundi ama Nyanwi si majina unayoweza kuhakikisha kwamba ni hai. Hili ni kizuizi kwa upelelezi” Siboyintore  alisema

Mwendeshamashtaka Mkuu nchini, Jean Bosco Mutangana alisema kwamba kama watuhumiwa ni watu kutoka nchi za ugeni lazima kufuata njia za kidiplomasia .

“ Na Wanyarwanda vilikuwa vigumu kuwafikisha mahakamani lakini tutafanya liwezekanalo,hatutashindwa hizi kesi”

Mwendeshamashtaka amesisiyiza inabidi ushirikiano na Burundi kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.