kwamamaza 7

Rwanda yataka kusaini kwa haraka mkataba wa ulinzi wa angani baada ya Burundi kutekeleza hili

0

Balozi wa Rwanda nchini Urusi, Jeanne d’Arc  Mujawamariya ametangaza Rwanda inasubiri kwa hamu kutia saini kwenye mkataba wa ulinzi wa angani.

Kwa mujibu wa chombo cha habari Sputnik, Balozi Mujawamariya amesema Rwanda ilimaliza kutimiza mahitaji yote kwa upande wake na inasubiri upande wa Urusi.

Balozi Mujawamariya

“ Kutakuwepo mkataba wa ulinzi wa angani kati ya Urusi na Rwanda. Itawezekana hivi karibuni. Mpira uko kwa uupande wa Urusi, tunasubiri watakachokifanya wenzetu”

Mujawamariya amesisitiza huu mkataba utasaidia kuhakikisha ulinzi wa angani.

Haya ni baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergeui Lavlov mwezi Juni Kutangaza kutakuwepo mkataba kuhusu ulinzi wa angani kati ya Rwanda na nchi yake.

Bunduki iliyotakiwa kununuliwa na Burundi

Hili ni baada ya Burundi  kununua Pantsir-S1 kwa kupambana na uvamizi wa angani.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.