Reli ya kutoka Mombasa kufika Nairobi ambayo serikali ya kenya imekwisha jenga hivi karibuni inachukuliwa na nchi za eneo la Afrika ya mashariki kama fursa nyingine inayostahili kuzalishwa mali, na hapa Rwanda haikufumba macho.

Jirani mwema akipata jambo jema nawe unaweza nufaika nalo, na haya ni sambamba na jinsi nchi za Afrika ya mashariki zitakaavyoweza kunufaika na reli ambayo imekwisha jengwa na Serikali ya Kenya

Reli hii ya SGR (Standard Gauge Railways) itaboresha ushirikiano kati ya nchi za eneo hili zilizoamua kujijumisha kwenye juhudi iliyoitwa,ushoroba/corridor ambako pia Rwanda ni mwanachama kama Waziri wa Uchumi, Amb Claver Gatete alivyojitangazia chombo cha habari cha Uchina cha Xinhua net.

Alisema “Ni mradi iliofikia lengo lake kwa hivyo Uchina ni wa kupongezewa”

Gatete anaendelea kusema kwamba nchi za eneo hili zitanufaika na reli hiyo, hususani za ushoroba wa kaskazini ambao unajumuisha nchi kama, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na pia ushoroba wa kati ambao unaanzia Tanzania, ukapitia Rwanda na Burundi utarahisisha uchukuzi wa watu na bidhaa.

Reli hiyo ya ulefu wa 480 km, iligharimu billion tatu na million mia nane za dola za Kimarekani, ilijengwa na Shirika la ujenzi la Uchina (China Road and Bridge Corporation), na 90% ya gharama yote ikiwa ni msaada kutoka China.

Reli hiyo ilizinduliwa tarehe 31 Mei, rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alisema kwamba reli hiyo ambayo ilipewa jina la ‘Madaraka Express’ itasaidia kubadili historia ya wa Kenya kwa kipindi cha miaka 100 itakayokuja.

Rais Paul Kagame alimpongeza rais wa Kenya kwa hatua hiyo aliyo piga. Kupitia ujumbe wake wa njia ya twitter alisema kwamba hatua hiyo inastahili pongezi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Faida nyingine ya Rwanda italingana na kuwa Rwanda inamiliki hekta 12 za ardhi kwenye bandari ya Mombasa ardhi ambayo Rwanda ilipewa mwaka wa 1986 na Daniel Arap Moi aliekuwa rais wa Kenya. Kulikuwa na kesi za mahakama nyingi juu ya ardhi hiyo ambapo Mwenyemali mkenya Salad Awale ambae anaendesha shughuli zake za Kibiashara Mombasa alikuwa akidai kwamba ardhi hiyo ni yake na kwamba ana vitambulisho.

Reli hii ambayo ilizinduliwa ni sehemu ya kwanza ya mradi wa reli ambayo itatoka Kenya ,ikapitia Uganda na Rwanda hadi Burundi, kwenye nchi zinazojumwika katika ushoroba wa kaskazini na kutakuwa nyingine ambayo itapitia pia Ethiopia na Sudani Kusini

Reli hiyo ambayo inakutanisha jiji la Nairobi na Mombasa, ambako magari ya mizigo amekuwa akitumia siku mbili lakini kwa hivi treni itakuwaikitumia masaa kati ya tano na nane kulingana na mizigo yake ikiwa ni watu ama mizigo ya kawaida.

Rwanda inaingiza bidhaa zake nyingi kupitia bandari za Mombasa na Dar Es Salaam ambako bidhaa zinazopitia bandari ya Dar Es Salaam ni 70% ya bidhaa zote zinazoingia Rwanda nyingi zikiwa zile zinazopitia meli ya India zikitoka Ulaya na Nchi nyingine za Azia.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.