Bunge nchini Rwanda, Alhamisi lilipitisha sheria ya uhalifu wa mtandaoni yenye nia ya kuisaidia sekta za kiserikali na binafsi kudhibiti uhalifu huo.

Bunge la juu lilipitisha muswada na kupeleka kwenye bunge dogo. Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi.

Sheria inalenga kulinda taarifa za serikali na binafsi na miundombinu dhidi ya uhalifu wa mitandaoni na mashambulizi ya mitandaoni, kwa mujibu wa Wizara ya habari na mawasiliano na Teknolojia ya Rwanda.

”kwa sasa tunashuhudia mashambulizi ya mitandaoni duniani kote. Mashambulizi ambayo yanatishia usalama wa uchumi na usalama wa taifa,” alieleza Agnes Mukazibera,mmoja mwa Wabunge baada kura.

Sheria itaisaidia serikali kufanya uchunguzi vitisho vyovyote na kushtaki dhidi ya vitendo hivyo katika taasisi binafsi na za umma na kuitetea nchi dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.

Mwaka 2016 Rwanda ilidhibiti zaidi ya mashambulizi ya mitandaoni 1,000 kila siku kabla ya kuleta madhara kwa walengwa,makampuni na taasisi,kwa mujibu wa Benki kuu Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina