kwamamaza 7

Rwanda yapiga marufuku bidhaa za kilimo asili ya Afrika kusini

0

 

Serikali ya Rwanda kupita wizara yake ya kilimo na ufugaji imepiga marufuku bidhaa za kilimo zenye asili Afrika Kusini zikiwemo nyama,mboga na matunda.Hili ni kujikinga ugonjwa wa Listriosis maarufu kama Kaba ulioko Afrika Kusini.

Waziri wa kilimo na ufugaji,Geraldine Mukeshimana kupitia tangazo amesema kuwa hairuhusiwi kuingiza nchini Rwanda bidhaa hizi hadi ugonjwa huu utolewe dawa nchini Afrika Kusini.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ugonjwa huu huvamia binadamu hasa wanawake wajawazito,watoto changa,wazee na mifugo kama vile ng’ombe,mbuzi,kondoo kwa kushambulia ubongo.

Baadhi ya dalili za ugonjwa huu kuna kushindwa kula,kupiga kimya,kushindwa kutembea na nyingine.

Ripoti ya mwaka 2017 inaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa wa Listeriosis 557 na  36 baadhi yao walifariki baada ya miezi 11.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.