kwamamaza 7

Rwanda yalaani uamuzi wa mahakama nchini Ubelgiji kuhusu mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi

0

Tume ya kupambana na mauaji ya kimbali nchini Rwanda (CNLG) imepiga marufuku uamuzi wa mahakama ya rufaa nchini Ubelgiji kwamba hiyo nchi yenyewe  haikuamua kuondoa wanajeshi wake  nchini  Rwanda wakati wa mauaji  ya kimbali dhidi ya Tutsi 1994 badala ya kunusuru waliokuwa wakiuawa.

Kiongozi wa tume hii  Dk. Jean Damascene Bizimana amepinga  huu uamuzi  kwa kusema ni wa kisiasa siyo wa kisheria.

“ Nafikiri kwamba uamuzi wa mahakama una msingi wa kisiasa siyo wa kisheria.Nawaza kuwa  hii mahakama inaogopa kuwa walionusurika huko Eto Kicukiro wataomba fidia”

 Mahakama imeamua haya baada ya miaka 14 walionusurika kufikisha kesi mahakamani nchini Ubelgiji wakishtaki serikali kushindwa kuwalinda Watutsi waliokimbilia  eneo laETO  Kicukiro mjini  Kigali wakati wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda.

Hata hivyo, mahakama tarehe 15 Juni mwaka huu iliamua wanajeshi wa Ubelgiji waliondoka nchini Rwanda kwa kutii amri ya Umoja wa Mataifa (YUNA).

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.