kwamamaza 7

Rwanda yalaani kuna mazungumzo ya siri na Burundi

0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ushirikiano, Olivier Nduhungirehe amepiga marufuku kuna mazungumzo ya kisiri kati ya Rwanda na Uganda kuhusu ushirikiano.

Haya ni baada ya Waziri wa Mambo ya Nje nchini Burundi, Ezechiel Niyibigira wiki iliyopita kutangazia Sauti ya Marekani kuwa kuna mazungumzo ya kisiri kati ya Rwanda na Burundi yanayolenga kuboresha ushirikiano.

“Hakuna mtu yeyote ambaye alizungumza na viongozi kwa upande wa Burundi. Hizi ni fununu na Ezechiel Niyibigira ama Willy Nyamitwe wanakubaliana name” Nduhungirehe  amesema

Huyu ameendelea akiuliza haya mazungumzo yalitokea wapi,lini na waliohudhuria.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Ezechiel Nibigira

Viongozi wa Burundi walionyoshea kidole Rwanda wakisema inastahili kuomba radhi kutokana na matendo yake mwaka 2015 na 2016.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi ulianza kuwa ovyo tangu mwaka 2015 ambako Burundi ilishtaki Rwanda kuwaunga mkono waliolenga kupindua utawala wa Rais Nkurunziza.

Kwa upande mwingine, Rwanda ilikanusha haya yote na kunyoshea kidole Burundi kwamba inawahudumia wale amabao wanataka kuharibu usalama wake.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.