Swahili
Home » Rwanda yajibu wasiwasi za DR Congo kuhusu mkutano nchini Angola
HABARI MPYA

Rwanda yajibu wasiwasi za DR Congo kuhusu mkutano nchini Angola

Waziri makamu kwenye Wizara ya  mambo ya nje nchini Rwanda, Olivier Nduhungirehe ameeleza inawezekana kuwa  DR Congo ilisikia kinyume na maana ya mpango  uliotangazwa wa kuwa kutakuwepo mkutano utakaozungumza kuhusu DR Congo siku za usoni nchini Angola.

Haya ni baada ya Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano nchini DR Congo, Leonard She Okitundu jumamosi kuzungumza na balozi wa Rwanda kuhusu mkutano utakaotokea Mjini Luanda,Angola.

Vyombo vya habari nchini DR Congo vilandika Okitundu alikuwa akitaka kujua mapana na marefu kuhusu hotuba ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron terehe 23 Mei kutangaza kwamba alizungumza na Rais Kagame kuhusu DR Congo.

Rais Kagame na Rais Macro wakizungumza na vyombo vya habari mjini Paris

Pia vimeeleza hili lilifanyika kuonyesha kwamba hakuna nchi yeyote yenye uwezo wa kuingilia mambo ya nchi nyingine kulingana na sheria za kimataifa.

“Haya ni hoja za Rais wa Angola kuwalika  marais wengine kwa kuzungumza kuhusu DR Congo. Rais Kagame kama kiongozi wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa atatii uamuzi utakaotolewa.Ni hayo tu ” ameeleza Waziri Nduhungirehe

Pengine, DR Congo ilisema Rwanda inalenga kutoa mchango katika mambo ya kumpindua Rais Joseph Kabila.

Waziri wa Mambo ya Nje  wa Rwanda Louise Mushikiwabo alitangazia France 24 kuwa haya mashtaka ni uongo mtupu.

Haya mashtaka yamezuka baada ya DR Congo kumkamata bi Desire Rwigema,Brigitte Safari Misabiro aliyekuwa mmoja mwa viongozi wakuu wa wanamgambo wa M23 akivuka mpaka kati ya Rwanda na DR Congo wilayani Rubavu.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com