kwamamaza 7

Rwanda yajibu Prof. Neirot aliyekosoa mkataba wake na Arsenal

0

Bodi kuu ya maendeleo nchini Rwanda (RDB) imejibu Prof. Lisa Neirot aliyesema kuwa mktaba wa Rwanda na Arsenal hautaza matunda.

Prof. Lisa Neirot aliye kosoa mkataba wa Rwanda na Arsenal

Prof. Neirot ambaye ni mwalimu chuo cha George Washington na mtalaam wa mambo ya matangazo ya bidhaa alitangaza kuwa hii namna ya uchumi ni ya kawaida kwa nchi zikiwemo Mexico, Bermuda, Alberta na Florida na kuongeza  Rwanda haitapata lolote.

Kwa kujibu haya, RDB imetangaza Rwanda inamiliki mbuga za wanyama tatu na kuwa watalii waliongezeka asilimia 6 mwaka 2017 kutokana na usalama wa ndani na huduma nzuri kwa watalii.

Pia RDB imepiga marufuku maoni ya Neirot kwamba makumbusho ya mauaji ya kimbali ni baadhi ya mahali pa utalii nchini.

“Makumbusho ya mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi hayajawahi kuwa baadhi ya mahali pa utalii, hayakufanyiwa matangazo ya namna hii, haitatikea kamwe” RDB imetetea

Hata hivyo, wengi mwa watu dunia nzima walikosoa huu mktaba kati ya Rwanda na Arsenal. Baadhi yao kuna wabunge nchini Uholanzi na Uingereza waliosema kuwa haya ni matumizi ovyo ya mali ya umma.

Kwa upande mwingine, RDB ilifafanua huu mkataba utasaidia kuongeza pato la utalii na mpira nchini Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.