kwamamaza 7

Rwanda yaishtaki Uganda kuwasaida wanamgambo watakayoishambulia

0

Kupitia barua ya ubalozi wa Rwanda nchini Uganda,Rwanda imeomba serikali ya Uganda kueleza kwa mapana na marefu kuhusu suala la kuwakamata Wanyarwanda na taarifa husika na kusajili wakimbizi asili ya Rwanda kwenye jeshi la RNC la Jenerali Kayumba Nyamwasa linalodhamiria kushambulia Rwanda.

Kwenye barua hii ubalozi wa Rwanda umetaja majina ya Wanyarwanda waliokamatwa kwa namna ambayo hawasiliani na wengine hata ubalozi wa Rwanda.

Hata hivyo, serikali ya Uganda inahakikisha kuwa kuna ushrikiano mzuri kati yao na Rwanda. Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Uganda,Amb.Patrick Mugoya amehakikisha kuwa walipokea barua hii na kuwa yaliyomo yatajadiliwa na viongozi mbalimbali kisha watangaze fikra zao kuhusu jambo hili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Patrick Mugoya ametangazia Chimpreports kuwa hili haliwezi kuharibu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na kusisitiza kuwa kuna ushirikiano mzuri kati ya Rwanda na Uganda.

Haya ni baada ya taarifa za kuwa Wanyarwanda karibu elfu ni wafungwa gerezani nchini Uganda kwa kutuhumiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.