Swahili
Home » Rwanda yahakikisha wanamgambo kutoka Burundi washambulia tena kusini
HABARI MPYA

Rwanda yahakikisha wanamgambo kutoka Burundi washambulia tena kusini

Msemaji wa Polisi nchini Rwanda, CP Theos Badege amehakikisha watu wenye bunduki ambao hawajajulikana kutoka Burundi  jana usiku wemeshambulia wilayani Nyaruguru, kusini mwa Rwanda mala nyingine.

Hawa wameiba mali ya wakazi ikiwemo vyakula,mifugo,nguo na fedha baada ya kupiga risasi nyingi kwa kubabaisha wakazi.

CP Theos Badege amesisitiza aliyosema kiongozi wa Kijiji huko, Francois Xavier Rubumba kwamba hawa wanamgambo wameiba mali ya wakazi kadhalika kisha wakaingia ndani ya mbuga ya Nyungwe na kuelekea nchini Burundi.

“ Yalikuwa ni kama majira ya saa tanu na nusu usiku,wamekuja na kupiga risasi,hawakuua mtu lakini wameiba familia 14 mali ikiwemo nguo za ikie na za kiume,kondoo kumi na  wawili, mbuzi wawili.”

“ Wameiba hata na fedha,wamewateka nyara wakazi tisa kwa kubeba mizigo yao ila wamewaachia huru”ameongeza

Huyu Kiongozi ameongeza kuwa jeshi la Rwanda limefika huko kutoa msaada ila hawajajua bado  taarifa zaidi.

“ Jeshi la Rwanda limewafuata mwituni Nyungwe ila hatujajua kama wamewakamata”

Kiongozi makamu kwa wajibu wa mambo ya kijamii wilayani Nyaruguru, Collette Kayitesi ameeleza hawezi kutangaza mengi kuhusu hili kwani wanausalama wanafanya ufuatiliaji wake.

“ Ni katika tarafa ya Nyabimata tena, wanausalama wanafanya ufuatiliaji wake, mimi sijajua mengi husika”

Shambulizi hili limetokea baada ya  siku zilizopita watu wenye bunduki kuwaua watu wawili na kujeruhi sita wakiwemo Katibu Mtendaji wa Tarafa ya Nyabimata, Vincent Nsengiyumva.

Wakazi walitangaza kuwa hawa wanamgambo walijigmaba kwamba walisha tawala hii tarafa na kuwa wakazi hawana budi kuungana mkono nao.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com