kwamamaza 7

Rwanda yafunguka kuhusu lawama za mkataba wake na Arsenal

0

Kiongozi wa Bodi Kuu ya Maendeleo (RDB) Claire Akamanzi amesema wanaokosoa mkataba wenye bei ya Euro miliyoni 30 kati ya Rwanda na Arsenal ni wale ambao hawatakii mema Rwanda ama hawaelewi mambo ya biashara.

Kupitia ukuta wake wa twitter, Akamanzi ameandika “Yeyote anayelaumu huu mkataba na Arsenal anaweza kuwa analenga maovu kwa Rwanda au hana habari yoyote kuhusu biashara”

Huyu amesisitiza huu mkataba utasaidia Rwanda kufikia lengo lake la kupata fedha kutoka $ miliyoni 404 hadi 800 mwaka 2024.

” Hatutapiga shabaha tunapoka kimya bila kufanya chochote.Haina budi kujulisha dunia nzima kwamba Rwanda ni mahari pa utalii”

Huyu kiongozi amesema haya baada ya mabunge wa Holland kumuomba Waziri wa Mambo ya misaada Kaag kufanya uchunguzi wa mkataba huu.

Wachezaji wa Arsenal wakiva jezi yenye ujumbe ‘Visit Rwanda’

Mmoja mwa hawa wabunge Isabelle Diks alisema hii ni jambo la kusikitisha kulingana na namna ambavyo nchi kama Rwanda inayotegemea misaada ya nje kutekeleza hili wakati ambapo dunia inakumbwa na ufukara.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.