kwamamaza 7

Rwanda yaamrisha wazungu 2 kurudi Ufaransa

0

Roger Patrick Claude Michel na mwenzake Jean Marc Roger Dimanche ambao ni wananchi wa Ufaransa wamerudishwa katika nchi ya uzazi baada ya kujiingiza nchini Rwanda kutoka Jamhuri ya demokarasi ya Congo bila vitambulisho. Tendo lilifanyika tarehe 13 Oktoba 2016 baada ya shirika la wahamiaji kuwapatia visa.

Inasemekana kwamba wafaransa hawa walikamatwa wakiwa kwenye mpaka wa Rwanda na Congo katika wilaya ya Rubavu. Walipigwa jela mnamo tarehe 22 Agosti 2016 baada ya kujaribu kuingia bila vitambulisho.

Shirika ya wahamiaji nchini Rwanda iliwaomba wageni kurudi Congo walipotoka ili kuomba rukhsa ya kuingia wakitumia mtandao wa intaneti nao wakakataa.

bahawe-visa-zibemerera-gusohoka-mu-rwanda
Roger Patrick na Jean marc walipewa vitambulisho vya kuwarudisha ufaransa

Kutokana na taarifa ya habari ya gazeti la Kigali today, wanaume hawa waliingia wakibebwa na gari la umoja wa mataifa ya Ulaya. Walipofika Kigali walikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi Kacyiru ili kutoa maelezo kuhusu tendo.

Baada ya kusikiliza kesi yao, Roger Patrick na Jean marc walipewa vitambulisho vya kuwarudisha ufaransa juzi.

Kulingana na sheria, waliadhibiwa faini ya milioni moja ya sarufu ya Rwanda kwa kila mmoja baada ya kukubali kosa la kuingilia nchi bila vitambulisho.

Théogène U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.