kwamamaza 7

Rwanda: Waziri mkuu aongoza mkutano wa kuadimisha siku ya Wafanyakazi wa Serikali wa Afrika

0

Waziri mkuu amefungua mkutano wa siku tatu wa kuadimisha Siku ya Wafanyakazi wa Serikali wa Afrika ( African Public Service Day) ambayo inaadimishwa mwezi Juni wa kila mwaka tangu 1994.

Katika maadimisho ya siku hii ambayo yana lengo kuwafanya wafanyakazi wa serikali kufikilia mchango wao wa kuendeleza kazi kwa kasi, Anastase Murekezi, waziri mkuu amegusia mambo mbali mbali ikiwemo umuhimu wa huduma nzuri na mchango wa vijana katika kuendeleza sekta ya kazi.

Amewakumbusha, katika hotuba yake, kwamba huduma nzuri ndio waafrika wanayotarajia kupata kwa kuwa ni haki yao siyo hisani kama rais Paul Kagame alivyosema wakati mmoja.

Waziri mkuu aliweka bayana kwamba, ili kuendeleza huduma nzuri kama inavyopendekeza malengo ya Afrika wa Mwaka 2063, wanapaswa kufanya kwa bidii na kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali ikiwemo sekta ya ustawi wa jamii, uchumi na hasa kuichunga mali ya umma kama ipasavyo. Kwa hili amepata fursa ya kuwaomba waliohudhuria mkutano huo kutoa ushauri wao kulingana na ujuzi wao na ukongwe wao wa jinsi Afrika inaweza kuindeleza sekta ya huduma nzuri kwa kasi.

Kuhusu wafanyakazi wa serikali amewahimiza kuwa mfano na kujiepusha na tabia ya kuchelewa chelewa kwa hapa na pale katika utoaji huduma. Amewahimiza pia kufanyakazi kwa ari na kujitolea ili waweze kuibadili Afrika bara lenye utawala bora, lisilo na rushwa, na lenye uchumi unaopanda kwa kasi.

Amependekeza pia kuwaongeza wataalam, kutenda kwa haki sawa na uchungaji mzuri wa mali ya umma kwa ajili ya kuendeleza utoaji wa huduma nzuri.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Jambo jingine ambalo waziri mkuu amewahimiza kutilia mkazo ni mchango wa vijana ambao utapewa nafasi muhimu katika maadimisho ya siku hii. Amesema kwamba kutowashirikisha vijana katika shughuli za kila siku ni kujidanganya sana kwa kuwa vijina wanajumuisha asili mia 60 za waafrika wote.

Kuwaongezea uwezo vijana, serikali zinapaswa kuwapa mafunzo maalum kulingana na hali ya kazi na hasa soko la ajira. Kwa hiyo serikali za Afrika zinapaswa kuimarisha misingi ya elimu ili kuilinganisha na malengo ya maendeleo. Wakiiga maagizo ya Nelson Mandela ambaye alisema “ Elimu ni Silaha Kubwa ambayo inaweza kutumiwa kuibadili dunia”

Mkutano huu wa kuadimisha Siku ya wafanyakazi wa srikala wa Afrika,ambao umeanza tarehe 21 Juni anatarajiwa kumalizika tarehe 23 Juni.

 

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.