kwamamaza 7

Rwanda: Waziri aliyedaiwa uhasherati aonekana hadharani baada ya miezi minne

0

Aliyekuwa Waziri wa miundo mbinu, James Musoni jana tarehe 13 Ogasti 2018 ameonekana hadharani baada ya miezi minne  Rtd.Capt. Patrick Safari, 47, kudai alimpokonya mwanamke wake, Imaculee Kayitesi aliyemuoa mwaka 2010.

James Musoni ameonekana akiwa na furaha machoni, akiangua kicheko kwenye kampuni za kuwania ubunge za chama tawala RPF-Inkotanyi wilayani Rulindo, kaskazini mwa Rwanda.

James Musoni akisalimiana na Kiongozi wa chama PDI

Huyu maarufu kama ‘Super Minister’ aliondolewa madarakani  mwaka huu kufuatia  madai ya  jina lake kuhusishwa na visa vya ngono na mambo mengine.

Rtd Capt. Safari alihakikisha kwamba  Waziri Musoni alimpachika mimba mke wake na kusababisha hasara kubwa kwa kuwa familia hii ilishindwa kulipa deni la benki sawa na  frw miliyoni 40 pamoja na kukataliwa kuja nyumbani kwake hadi alipoenda kulala hotelini.

Musoni hakueleza lolote kuhusu haya madai, alifukuzwa mwezi huo ambako wengi  walikuwa ni kwa ajili ya visa vya kufanya ngono.

Waziri James Musoni alikuwa madarakani  tangu mwaka 2005 ambako aliongoza wizara mbalimbali.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.