kwamamaza 7

Rwanda: UNHCR yaomboleza familia ya mkimbizi asili ya DR Congo aliyefariki wakati wa mapambano na polisi

0

Mkurugenzi wa Shilika la kuwahudhumia Wakimbizi(UNHCR) nchini Rwanda, Ahmed Baba Fall ameomboleza familia ya mkimbizi aliyefariki kwa kujeruhiwa mno wakati ambapo kundi la vijana lilikuwa likipambana  na jeshi la polisi waliokuwa kwenye ulinzi katika kambi ya Kiziba,magharibi mwa nchi.

Baba Fall amesema ana masikitiko kutokana na huu msiba na kuwa anaunga mkono familia ya malehemu na wakimbizi asili ya DR Congo kwa ujumla.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“UNHCR inasikitishwa na na msiba huu,inaunga mkono familia yake na wakimbizi wengine kwa ujumla” Baba Fall amesema

“ Tuliwaambia wakimbizi mala nyingi  kutii sheria za ndani nchini Rwanda na kutatua masuala yao kupitia mazungumzo.Pia,tuliwaomba viongozi kufanya ufuatiliaji  wa hili jambo kwa uzito wake”

Huyu kiongozi ameongeza wakimbizi wana haki ya kurudi kwao wakitaka

“Tunawataka wakimbizi kuamua kuhusu hili jambo bila kusikiliza fununu ama habari zisizo na msingi”

UNHCR imeeleza tangu tarehe 30 Aprili 2018 wakimbizi walianza vitendo vya kupambana na polisi hasa makundi ya vijana yaliyokuwa yakitupa mawe.Hili lilifanya polisi kutumia mbinu zozote kupambana na haya maandamano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

UNHCR imesisitiza Polisi ya Rwanda itaenedelea kujadili mambo ya usalama  ili kuleta utulivu kwa kurahisisha mawasiliano katika kambi ya Kiziba.

Ghasia na maandamano vilianza mwezi Februari ambako wakimbizi walikuwa wakisema maisha yao yangali hatarini kutokana na kupunguza chakula cha kila siku.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya maandamano yalisababisha vifo vya watu 11 kama ilivyohakikishwa na Polisi ya Rwanda ila baadhi ya waliokuwa chanzo cha haya 44 walikamatwa.

Kambi ya Kiziba inawahudhumia wakimbizi asili ya DR Congo 1720 tangu mwaka 1996.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

[xyz-ihs snippet=”google”]

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.