kwamamaza 7

Rwanda-Ufaransa: Je, mabadiliko yataleta ubalozi mjini Kigali?

0

Yeyote anaweza kujiuliza kama jitihada za kuboresha ushirikiano kwa  rais wa Rwanda Paul Kagame na  Emmanuel Macron wa Ufaransa zitayafikia mengi yakiwemo kuanzisha tena uabalozi mjini Kigali.

Matumaini yanaongezeka unapofikiria aliyoyasema Kiongozi wa Ufaransa kwa mambo ya nje nchini Rwanda,Etienne de Souza.

Huyu kiongozi alielezea vyombo vya habari kuna tumaini za kuboresha ushirikiano hata kama hatua zilzopigwa ni chache.

“Tunajaribu kutumia fursa yoyote tunayo,kulikuwepo wakati ambapo nchi hizi mbili ziliapata fursa.Nafikiri kuwa tungali njiani ya kubadili mambo” de Souza alisema

Pia, kwa maneno ya wahenga wengi nchini Ufaransa kama yule Mwandishi Jean-François Dupaquier, huu ni wakati wa kuboresha ushirikiano kati ya  Rwanda na Ufaransa.

Kupitia barua aliyomuandikia Rais Macron alisema haina budi  sauala hili litolewe suluhisho miezi tano ya usoni.

“Namna gani Paris inaweza kushirikiana na Kigali? Cha muhimu ni ukweli.Kunahitajika uchunguzi wa maandishi ya ikulu kati ya mwaka 1990-1994”aliandika

“Kutimiza hili kitakuwa kitendo cha Rais Macron kutekeleza aliyoahidi Ufaransa” Dpaquier aliongeza.

Rais Kagame atafika nchini Ufaransa tarehe 24 Mei 2018 kwa kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu teknolojia(Viva Tech).

Inatarajiwa kuwa Rais Kagame atazungumza na Rais Macron kabla kumkuta Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Facebook Mack Zuckerberg.

Ufaransa hauna ubalozi nchini Rwanda tangu mwaka 2015  baada ya Michel Flesch kumaliza mamlaka yake.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Ufaransa ulianza kuwa mkia wa mbuzi tangu mwaka 1994 ambako Rwanda ilishtaki Ufaransa kushiriki katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi.Hata hivyo,Ufaransa ulikanusha haya mashtaka yote.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.