kwamamaza 7

Rwanda: Serikali yauza mnada mashini za kuanda sigara za kiwanda cha familia ya Rwigara

0

Ofisi ya kodi nchini Rwanda (RRA) jana jumatatu  imeuza mnada mashini za kuanda sigara za kiwanda Premier Tobacco Company ( PTC) cha familia ya Rwigara frw biliyoni moja na miliyoni 797.

Mfanyakazi wa mahakama Me Vedaste Habimana ameuza hii mali ili kulipa fedha  frw biliyoni sita ambazo  hiki kiwanda hakikulipa serikali ya Rwanda tangu mwaka 2012.

Kwa niaba ya familia ya  Assinapol Rwigara, bintiye  Anne Uwamahoro Rwigara amesema hawakubaliani na hii bei kwa kusema ni “duni”

“ Sisi kama kiwanda cha PTC hatutakubaliani na bei hii”

Huyu amesema bei iliyotoa inastahili kuwa mala tano ya mashini zilizouzwa.

Me Habimana ameeleza hawa hawana haki za kukataa hii bei kwani hawakuweza kutoa bei yao. Hata hivyo, Anne Rwigara amekanusha haya kwa kueleza hakuweza kuingia ndani ya kiwanda ili kutoa bei ya hizi mashini za kuandaa sigara.

Kwa sasa, familia ya Rwigara imeisha lipa frw biliyoni mbili na miliyoni 309 tu.

Mkurugenzi wa RRA alisema kuwa mnada utaendelea  hadi hii familia ilipe frw  biliyoni sita.

Pamoja na hayo, mama mazi wake Adeline Mukangemanyi Rwigara aliyegerezani alisikika mala  nyingi akisema kwamba hawana deni lolote la serikali ya Rwanda.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.