kwamamaza 7

Rwanda: Serikali yatangaza namna ya kutatua suala la uhaba wa simenti

0

Wizara ya  Biashara na Viwanda imewataka wafanyabiashara kuingiza simenti kutoka nchi za nje kama  Kenya, Uganda na Tanzania  ili kueweza kutatua uhaba wa  simenti ulioko nchini tangu mwezi Februari 2018.

Kwenye mazungumzo na Watangazaji,Wizara  imesema  kuagiza simenti kutoka nchi za nje ni moja mwa mbinu ambazo zitasaidia kuziba pengo la uchache na ongezeko la bei la simenti nchini.

Kwenye mpango huu, inatarajika kwamba Toni 30,000 zitaagizwa mwezi huu,takwimu ambazo ni kinyume na mwezi uliopita ambapo Toni 20,000 ziliagizwa.

Uhaba wa simenti ulijitokeza kutokana na kazi za ujenzi unaoendelea kwenye kiwanda cha simenti Cimerwa unaolenga kuongeza uwezo wake.

Waziri Vincent Munyeshyaka ameeleza kazi za ujenzi zitamalizika mwezi huu na kuwa Cimerwa itakuwa na uwezo wa kuanda Toni 500,000 badala ya 380,000

Takwimu za hii wizara zinaeleza asilimia 45 za simenti inayotumiwa nchini inatoka nchi za nje.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.