kwamamaza 7

Rwanda: Serikali imeanza mpango wa kutoa vitambulisho kwa wakimbizi asili ya DR Congo na Burundi

0

Serikali ya Rwanda  jana tarehe 30 Ogasti imeanzisha mpango wa kuwapatia vitambulisho kwa wakimbzi asili ya DR Congo na Burundi kwa kuwawezesha kupata huduma mbalimbali nchini humo.

Waziri kwa wajibu wa wakimbizi, Jeanne d’Arc De Bonheur na Kiongozi wa Shilika la Kimataifa la Kuwahudhumia Wakimbizi (UNHCR), Ahmed Baba Fall wameanzisha huu mpango kwa kutoa vitambulisho kwa wakimbizi 2,761 mjini Kigali na kuendelea nchini kote.

Ahmed Baba Fall akitoa vitambulisho kwa wakimbizi

Waziri De Bonheur amesema huu mpango wa kutoa vitambulisho utawasaidia wakimbizi kupata huduma nyingine kama vile kutembea nchini, kazi na kushiriki katika miradi mingine ya maendeleo nchini.

Takwimu za Wizara ya Wakimbizi zinaonyesha kuwa  kuna maelfu 153 ya wakimbizi kutoka DR Congo na Burundi.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.