kwamamaza 7

Rwanda na Kongo zayafikia makubaliano ya Ushirikiano katika nyanja muhimu

0

Waziri wa Fedha Claver Gatete amesema kwamba makubaliano ambayo nchi hizo mbili ziliyafikia atasaidia kukuza ushirikiano wa pamoja wa mipango ya Uchumi na hata ya kifedha.

Makubaliano yaho ambayo yametiwa saini Jana kati ya Rwanda na nchi ya Kongo Brazzaville yanatoa mwongozo ambao nchi hizo mbili zitaufutia kwa kushirikiana katika nyanja muhimu zilizotajwa. Yatajumuisha hususani shughuli za Takwimu, mipango ya nchi, uchungaji wa mali ya umma, mfumo wa bajeti na utozaji ushuru.

Rwanda imekuwa ikisimamiwa na waziri wa fedha na mipango ya uchumi Amb. Claver Gatete na kwa upande wa Kongo Callixte Nganongo waziri wa Fedha na Bajeti na hata Ingrid Olga Ebouka Babakas waziri wa mipango na shughuli za takwimu na hata uingiaji katika mashirika ya kimataifa baina ya nchi jirani za eneo la karibu (regional integration).

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amb. Gatete Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi amesema “ tunapaswa kuwa na ushirikiano katika shughuli zote za mipango na hata utekelezaji wa bajeti kutoka ngazi za uongozi kuu hadi za chini ili kutusaidia kujua ikiwa mgawanyiko wa bajeti unafanyika kulingana na mwongozo wa maendeleo ya nchi”

Gatete aliongeza hata kuwa makubaliano hayo yatujumuisha sekta ya mipango ya kifedha hususani kati ya mabenki, bima na hata kujadili na masoko ya mali.

Nchi hizo mbili ziliweka kipaumbele desturi ya kuigana kati yazo bila ya kuiga mifumo ya nchi za nje ya Afrika.

“Kilichoweza kufanyika nchini Rwanda hata na Kongo inaona kwamba kinaweza fanyika kwake kulingana na hili kutawekwa kundi la watalaam litakalofuatilia utekelezaji wa makubaliano haya” asema Gatete.

Waziri wa Mipango, shughuli za takwimu na hata uingiaji katika mashirika ya nchi za kimataifa za eneo la karibu alisema kwamba hatua ile ilianzia mwaka uliopita katika mkutano wa wakuu wa nchi na kuongeza kwamba ni wakati wa kuacha maneno na kuendelea na vitendo”.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.