Home HABARI Rwanda na Congo katika mabishano kwa ajili ya matokeo ya ziwa Kivu
HABARI - March 22, 2017

Rwanda na Congo katika mabishano kwa ajili ya matokeo ya ziwa Kivu

Uongozi wa vituo tofauti vya Rwanda na Congo wanaofanya utafiti kuhusu ziwa Kivu, husema yakuwa mabishano yanayo onekana kwa kuchangia matokeo huenda kutatuliwa.

Tatizo hilo huonekana sana wakati wa kuvua samaki na mengine yanayo liwa kutoka ziwa hilo.

Mradi wa utafiti ujulikanao kwa jina la SUSFISH utafanywa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Rwanda pamoja na kituo cha ufugaji na ukulima RAB hapo ni upande wa Rwanda, na upande wa Congo ni chuo kikuu ISP Bukavu, na hapo wanaamini suluhisho la matatizo hayo.

Munyemana Gerard, ni mmoja wa wavuvi katika ziwa Kivu, anasema ya kuwa wanapata tatizo wakati wa kuchangia mavuno kutoka ziwa Kivu kama samaki kwa sababu hawajui wapi sehemu gani, na wakati mwengine unakuwa wanavuka hata mipaka.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kamanzi Emmanuel, kiongozi wa EDCL anasema watachunguza matokeo ya samaki kutoka ziwa Kivu na matumizi yake, asema ziwa Kivu ni maliasili ya nchi zote mbili eti ni lazma kutumika kwa ushirikiano kwa kutafuta mafanikio bila kushwana sababu za samaki na mengine.

Eti “Mara nyingi tulikuta swala kati ya wavuvi wa nchi zote mbili, kuwa tunakwenda kufanya utafiti, kila upande utajua nafasi kuna matokeo mazuri, na hapo kila upande utajua sehemu nzuri kwa uvuvi na hakutaonekana tena mabishano”.

Ziwa Kivu ni maliasili kati ya Rwanda na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ila uchumi ulio ndani huleta mabishano kwa sababu ya kutojua upande wa Rwada na Congo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.