kwamamaza 7

Rwanda na Benin zafikia makubaliano ya pamoja ya huduma za safari za ndege

0

Rwanda na Benin zasaini mkataba wa kuanza idara ya safari za ndege ambapo Rwandair imezindua idara mpya itakayoendesha shughuli zake mjini Cotonou jana tarehe 1 Agosti. Hili limefikiwa baada ya Rwanda kupewa haki ya kuendesha shughuli za kampuni yake ya ndege (RwandAir) kwenye ardhi ya Benin kwenda nchi nyingine yaani ( Seven freedom rights).

Makubaliano hayo ya pamoja ya huduma za safari za ndege anaeleza kwamba safari zitakuwa zikiendeshwa kati ya miji ya Abidjan, Brazaville, Douala, Libreville, Bamako, Dakar na Conakry kulingana na tarifa alizoipa the NewTimes ya Rwanda Yvonne Manzi Makolo makamu Kiongozi mkuu .

Waziri wa mambo ya nje ya nchi, Mushikiwabo Louise amesema kwamba makubaliano haya yalipigiwa saini kwa ajii ya kuendeshwa na maadimisho ya siku ya Uhuru ya 57 ya nchi ya Benin.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alisema pia  kuwa Benin itakuwa na asilimia 51 hivi Rwanda nayo ikiwa na asilimia 49 yake ya mtaji.

“tumekuwa tukitaka kupafanya Afrika ya Magharibi nyumbani kwetu na tulilifikia kwa kupachagua Benin n ”

Waziri wa mambo ya nje wa Benin Aurelien Agbenonci, alisifu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na kuongeza kwamba RwandAir ni fahari kwa wakazi wa bara la Afrika.

“wafanyakazi wa idari hiyi watakuwa mchanganyiko wa wanyarwanda na wabenin na tunatarajia kuongeza vifaa vya kiwanja kwa ajili ya kukiinua kwa kiwango cha kimataifa. Hii itaifanya kampuni ya RwandAir kustawi katika eneo hili la Afrika” asema

Kampuni ya RwandAir itaendelea kufanya safari zake kutoka Kigali hadi Kotonou wakati ambapo safari hizo za pamoja zitaisaidia kufika maeneo ya Afrika ya Mashariki, magharibi na mashariki ya kati na hata Ezia.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.