Swahili
Home » Rwanda: Mwanamke amuua mwenzake asili ya Kigoma, Tanzania kwa kutumia mpanga
HABARI MPYA

Rwanda: Mwanamke amuua mwenzake asili ya Kigoma, Tanzania kwa kutumia mpanga

Mwanamke kwa majina Jacqueline  Nyiraminani,31,  mkazi Wilayani Rusizi kusini  magharibi mwa Rwanda,amemuua mwanamke kutoka  Kigoma,Tanzania, Yozabela Nazaleta Dastani,57, kwa kutumia mpanga.

Kiongozi wa kijiji huko, Callixte Kamanzi amehakikishia Bwiza.com tukio hili limetokea jana tarehe 19 Julai na kuwa tangu mwezi Aprili alianza kuonyesha dalili za kuwa katika hali ya wenda wazimu ila hakupata matibabu kwenye hospitali rasmi.

 “Ni ukweli huu msiba umetokea, huyu Nyiraminani alianza kuonyesha  dalili za uenda wazimu. Huyu Mtanzania alikuwa anamtibu tangu walipokuwa mjini Kigali kisha wakajaa huku Kamembe” amesema Kamanzi

“ Alikuwa ameisha(Nyiraminani) mlipa frw elfu 80, huyu daktari wa kienyeji alikuwa anataka kurudi mjini Kigali na alipoomba fedha nyingine,Nyiraminani amemua chumbani na akarudi akiwa na mpanga mikononi akamtema” ameongeza

Kiongozi wa wilaya ya Rusizi, Ephrem Kayumba ameeleza  haitakuwa rahisi kumzika Dastani kutokana na kuwa hana vitambulisho kamili.

“ Haitakuwa rahisi kumzika, isipokuwa kitambulisho kwamba ni mzaliwa wa Kigoma, hakuna taarifa husika nyingine. Kwa msaada wa Ofisi za uhamiaji tutajaribu kutafuta kama kuna wanafamilia wake”

Nyiraminani alikuwa ni daktari kwenye hospitali ya Gihundwe na kwa sasa amekamatwa na kufungwa kwenye kituo cha polisi cha Kamembe.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com


 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com