kwamamaza 7

Rwanda: Mpinzani alaani kuunda kundi la kigaidi

0

Mwenyekiti na Kiongozi wa chama cha upinzani, Ingabire Victoire amekanusha taarifa zilizoenea nchi nzima kwamba alipatikana akisajili watu watakaofanya fujo nchini sawa na ‘Arab Spring’.

Ingabire ameambia VOA, hizi taarifa ni uongo mtupu na kuwa zinalenga kumpaka masizi.

“ Nilisema nitajenga nchi yangu kwa njia ya amani. Mimi sina kundi la kigaidi. Hawawezi kuniacha baada ya kunikuta nikifanya vitendo vya kigaidi,” Ingabire amesema

Amesema taarifa hizo zinalenga kumharibia jina na kuwa angali tayari kujadiliana vilivyo na vyombo vya habari vilivyotangaza habari hizo.

“ Nimemuomba mwanasheria wangu kuwandikia waliotangaza zile taarifa ili kurekebisha. Wakikataa, tutatumia mahakama.” Ameongeza

Hata hivyo, Ofisi Kuu ya Upelelezi Uendeshamashtaka (RIB),jana ilitangaza kuanzisha upelelezi juu ya madai hayo.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.