kwamamaza 7

Rwanda: Maseneta waomba maelezo kuhusu matatizo yalimo barabarani

0

Dkt. Alexis Nzahabwanimana, Katibu wa Serikali katika wizara ya Miundombinu idara ya uchukuzi ameahidi maseneta kwamba watafuatilia matatizo yaliopo na mbayo ni tishio kwa usalama wa barabara.

Alipokuwa akieleza matatizo yaliyoko kwenye barabara kama pingamizi kwa sekta ya uchukuzi mbele ya maseneta wa bunge aliahidi kwamba matatizo yaliyoko kwenye barabara ambayo ni rangi inayopakwa kwenye barabara hasa sehemu ya kuvuka kwa miguu(zebra crossing) na hata matuta ya barabara(road humps) atafuatiliwa na kutafutiwa suluhu.

Seneta Jean Damascene Ntawukuriryayo aliuliza juu ya matuta yanayowekwa kwenye barabara kama yanajaza viwangongezi vya kimataifa na hata marangi yanayopakwa kwenye barabara na akajiwaza ikiwa rangi hiyo huwa si bandia.

Kufutia hili Dr Nzahabwanimana aliahidi kwamba watajitolea kufuatia matatizo hayo kwa karibu kwa kuwa yangekuwa hatari kwa usalama wa barabara. Aidha anakiri kuwepo kwa zile zisizokidhi viwango na kuongeza kwamba wanapoziona hizo wanajaribu kuzikosoa hadi sasa matuta ya barabara yanayokidhi vigezo vya kimataifa ni yale yaliyoko sehemu za Ku Kabindi.

Kuhusu ubora wa rangi zinazopakwa kwenye barabara napo alikiri kwamba kuna aina tofauti kulingana na ubora na kuongeza watalitilia maanani wakati wa kupigania masoko.

“tumekwisha gundua kuwa kuna rangi zinazodumu mda mrefu na zile zinazofutika kwa urahisi hususani mjini wa Kigali. Tumewaomba ngazi husika kufuatilia tatizo hili kwa karibu kwa kulifanyia uchunguzi, na kuweka masharti muhimu katika vitabu vya kupiagania masoko ili ije ikawa rahisi kuchunguza kwamba kazi ilifanyika kama ipasavyo” asema Dkt. Nzahabwanima

Ikiwa rangi ya barabara imepakwa vizuri, hii hupunguza hatari ya ajari za barabara, hususani sehemu ya kuvukia kwa miguu(zebra crossing)

Dr Nzahabwanimana aliahidi kwamba kuna mabadiliko kadhaa ya kanuni za kuadhibu utumiaji wa barabara kinyume na sheria yanayoendelea. Na hii itasaidia kupunguza hatari za usalama wa barabara.

Mara nyingi watumizi wa barabara, abiria na wendesha magari hulalamika kutokuwepo kwa saini za barabara na rangi huwa zimefutika. Kwa bahati nzuri Katibu huu Dr Nzahabwanimana aliahidi kwamba watalitolea suluhu tatizo hili hivi karibu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.